Maseno University Repository

Uchanganuzi wa uwasilishaji wa kifo katika mashairi teule ya Kiswahili

Show simple item record

dc.contributor.author ODONGO, Fredrick Orinda
dc.date.accessioned 2019-01-24T09:21:19Z
dc.date.available 2019-01-24T09:21:19Z
dc.date.issued 2014
dc.identifier.uri https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/1114
dc.description Masters' Thesis en_US
dc.description.abstract Kifo ni swala zito na linaloibua hisia zaidi. Uwasilishaji wa dhana ya kifo katika tanzu anuwai za fasihi huwa kwa namna tofauti. Katika ushairi kifo huibuliwa kwa lugha ya pekee yenye mnato wa hisia na mashiko zaidi. Ushairi hutumia lugha ya mkato na mapigo ya sauti yanayovutia na kunata pindi yanapowasilishwa kupitia kughani, usomaji na ukariri. Uchambuzi mwingi wa dhana ya kifo katika ushairi wa Kiswahili uliwahi kufanywa katika ushairi mbolezi ambao ni wa kisimulizi lakini swala hili katika ushairi andishi hutajwa tu kwa ufinyu wala haushughulikiwi kwa kina. Utafiti huu ulichambua uwasilishaji wa kifo katika mashairi teule ya Kiswahili. Uchambuzi huu ulifanywa kwa malengo ya; kutambua na kueleza taswira ya kifo; kubainisha visababishi vya kifo; na kuchunguza utata unaojitokeza katika ufafanuzi wa dhana ya kifo kama wanavyodhihirisha wasanii katika mashairi teule ya Kiswahili. Malengo haya yalifikiwa kwa kuzingatia mashairi matatu teule; Inkishafi, Mwana Kupona na ‘Usiniuwe’ katika diwani ya Sauti ya Dhiki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia kama ilivyofafanuliwa na Georg Lukacs (1938). Mihimili ya nadharia hii iliyotumika ni pamoja na tajriba ya mwandishi, historia ya jamii, muundo wa kazi, vielelezo na lugha. Utafiti ulikuwa wa kimaktaba. Mtafiti aliteua matini tatu za ushairi wa Kiswahili na kujikita maktabani na kuzichambua kwa kina huku akirejelea malengo ya utafiti. Uteuzi ulifanywa kimaksudi kwa kuzingatia usawirishaji wa dhana ya kifo. Muundo wa uwasilishaji data ulikuwa wa kimaelezo. Kupitia mihimili ya nadharia ya uhalisia, utafiti huu ulibaini kuwa; taswira ya kifo kulingana na mashairi teule ni pamoja na dhoruba ya kifo, kifo kinatamausha, uchungu wa mauti, kifo ni hatima ya kila kiumbe, kifo kina upweke, kifo si mwisho wa maisha na kifo kina ukatili. Usawiri wa kifo pia hujikita katika mazingira ya mtunzi ambayo hujitokeza katika vipengee vya wakati, dini au utamaduni na lugha. Aidha, kifo ni kitu kilicho na chanzo chake ikiwa ni Mungu, shetani na mtu. Utafiti huu ulidhihirisha kuwa hakuna mpaka bayana baina ya kifo na uhai hivyo mwanadamu anajikuta katika mkanganyiko wa kuishi huru duniani kwa hofu ya yatakayompata akhera. Utata huu hujitokeza katika kuelewa mwanzo na mwisho wa maisha, maisha baada ya kifo na uwezo wa kuzungumza na Mungu katika ufu. Utafiti huu ulihitimisha kuwa kifo ni hatima ya kila kiumbe na ni vema mwanadamu kukikubali na kuwa radhi nacho kwani huletwa na nguvu za kimaumbile nje ya uwezo wake. Akiishi mwanadamu, huwa yu mbioni akingoja kifo na ahera kwa kutegemea alivyoishi duniani. Ni mapendekezo ya utafiti huu kuwa kifo ni kiungo cha maisha kinachofanya uhai kuthaminiwa zaidi. Uwepo wa kifo hupatia maisha maana na ukosefu wake huyafanya kukosa kufasiriwa. Kutokana na utata wa dhana ya kifo, ni muhimu utafiti zaidi ufanyike kwa kuzingatia dhana ya uhai ili kuweka mwangaza zaidi kuhusu mpaka baina ya kifo na uhai na chanzo cha kifo; na utafiti linganishi ufanywe ili kubainisha taswira ya kifo katika tanzu nyinginezo za fasihi. en_US
dc.language.iso en_US en_US
dc.publisher Maseno University en_US
dc.subject Mashairi teule en_US
dc.title Uchanganuzi wa uwasilishaji wa kifo katika mashairi teule ya Kiswahili en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Maseno University Repository


Browse

My Account