• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uchanganuzi wa Athari ya Mageuzi ya Maneno kwenye Muundo wa Sentensi ya Ekegusii

    Thumbnail
    View/Open
    document.pdf (254.8Kb)
    Publication Date
    2019
    Author
    Wilfrida Kemuma Momanyi, Beverlyne Asiko Ambuyo, Rocha Mzungu Chimerah
    Metadata
    Show full item record
    Abstract/Overview
    Tasnifu hii inachanganua athari ya mageuzi ya maneno kwenye muundo wa sentensi sahili ya Ekegusii ikiangazia sheria na kanuni zinazotawala mageuzi hayo. Mageuzi ya kisintaksia huleta mabadiliko mengi katika sentensi asili. Utafiti huu ulichunguza na kuchanganua athari ya haya mageuzi kwenye muundo wa sentensi. Utafiti huu vilevile ulishughulikia viambajengo vya sentensi sahili ya Ekegusii kwa kudhihirisha kanuni mahususi zinazotawala muundo wa sentensi hiyo. Misingi ya kinadharia ya utafiti huu ni Sintaksia Finyizi kwa mujibu wa Chomsky. Data ilikusanywa maktabani kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi. Mbinu za maelezo zilitumika katika kuwasilisha data. Vijenzi vya sentensi sahili ya Ekegusii na dhana ya ugeuzi yanashughulikiwa ambapo majopo leksika na majopo amilifu yamejadiliwa kwa kina. Dhana ya ugeuzi na aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii pia imeshughulikiwa. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba mageuzi yanayofanyiwa muundo wa sentensi hayabadilishi maana ya sentensi asili. Matokeo na mahitimisho ya utafiti wetu yanadhihirisha kwamba, suala muhimu linalojitokeza ni kuwa kanuni geuzi zinasababisha mabadiliko katika muundo wa sentensi ingawa maana ya sentensi hubaki ile ile. Pili ni kuwa mageuzi hayafanyiki kiholela; hufuata utaratibu unaokubalika na kutawaliwa na kanuni mahususi. Mwisho ni kuwa utafiti huu unapendekeza kuwa dhana ya mageuzi ya kisintaksia ishughulikiwe katika lugha nyinginezo kwa kurejelea sentensi ambatano na kwa nadharia nyinginezo za kisasa. Utafiti huu utawafaidi waundaji wa mitaala katika lugha ya Ekegusii. Vile vile, utafiti huu utaweka msingi bora katika eneo la isimu linganishi miongoni mwa watafiti wengine mbali na wale watakaoitafitia mada hii katika lugha nyinginezo. Matokeo ya utafiti huu yatachangia katika kuelewa zaidi ubainishi wa miundo mbalimbali ya sentensi za kibantu na kuwafaidi walimu katika ufunzaji wa sintaksia ya kibantu na hasa katika lugha ya Ekegusii.
    Permalink
    https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/2944
    Collections
    • Department of Kiswahili & Other African Languages [38]

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Browse

    All of Maseno IRCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Statistics

    View Usage Statistics

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback