• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Mabadiliko katika Umbo la Ushairi na Athari zake katika Ushairi wa Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    15_07_Indede12.pdf (94.26Kb)
    Publication Date
    2008
    Author
    Florence Ngesa Indede
    Metadata
    Show full item record
    Abstract/Overview
    Mwanadamu amejaribu kwa vyovyote vile kuvumbua na kunyumbua mambo mapya ambayo yataleta mvuto na kupimia akili yake kiubunifu katika hali ya kutaka kutangamana zaidi na binadamu mwenzake au kutaka kuelewa zaidi ulimwengu wake. Ndiposa washairi wengi wa kisasa wanashikilia kwamba ulimwengu unabadilika na hivyo utamaduni wa ushairi lazima ubadilike pia asemavyo Mazrui (1988: viii): ... utamaduni hauna budi kubadilika maadamu uchumi na siasa za nchi zaendelea kubadilika. Mwelekeo huo unasisitizwa katika mjadala wa Wangari Mwai (1988: 5) anayeonyesha kuwa washairi wa kisasa wanaeleza kwamba fasihi hubadilika katika umbo na maudhui na kwa hivyo ushairi wa Kiswahili sharti uruhusu mabadiliko yanayotokea katika ushairi huru. Katika utangulizi wa swala la “Ushairi, Lugha na Mawazo”(“Poetry, Language and Thought”) Martin Heidegger (1971: xi) anazua swala la tofauti iliyopo kati ya mfikiriaji mshairi na mshairi mfikiriaji; kwamba ili kuwa mshairi mkomavu kuna ufikiriaji ambao mshairi lazima akamilishe. Ufikiriaji ulio na usafi, uzito na umoja wa ushairi. Uwazaji wa kiwango hiki huongezea ubora na utaalamu wa lugha ya ushairi. Fikra kama hizi si za kiajali bali zinakwenda sambamba na ukuaji wa maono ya washairi kwani mshairi alazimika kuzungumzia maudhui ya kiungu, bahari, mawingu, milima, maovu, maafa nk Hiki ni kiwango cha juu cha ufikiriaji na uwazaji unaozungumzia mambo ya kidhahania kuwasilisha uhalisia.
    Permalink
    https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/3039
    Collections
    • Department of Kiswahili & Other African Languages [38]

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Browse

    All of Maseno IRCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Statistics

    View Usage Statistics

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback