Show simple item record

dc.contributor.authorINDEDE, Ngesa Florence
dc.date.accessioned2021-10-30T09:23:37Z
dc.date.available2021-10-30T09:23:37Z
dc.date.issued2007
dc.identifier.urihttps://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/4295
dc.descriptionPhd Thesisen_US
dc.description.abstractLugha ni chombo cha mawasiliano ambacho hakiwezi kuepukika katika uwanja wowote ule palipo na maongezi hasa mahubiri. Lugha na dini vina historia ndefu kimahusiano hasa tunaporejelea umuhimu na uarnilifu wa lugha katika bibilia. Kwa upande mwengine lugha kitamathali imechukuliwa kuwa ya kimsingi sana katika dini. Hii ni kwa sababu, lugha tamathali ni lugha atharishi ambayo huathiri hisia za watu, huingia katika fikra zao na kuchochea mawazo yao. Miongoni mwa tamathali mbalimbali zikiwemo vinyume, methali, isitiara na nyinginezo, sitiari na tashbiha zina uwezo na kipawa cha kisaikolojia kinachoashiria undani na uimarishaji wa mawasiliano. Hiki ndicho kichocheo kinachowasukuma wanafalsafa na wanauchanganuzi wa semi kuchanganua dhima ya lugha ya kidini kama mbinu ya mawasiliano. Kwa rnisingi hii utafiti huu unalenga maturnizi ya lugha ya kitamathali katika mahubiri ya dini ya kikristu ambapo sitiari na tashbiha ndizo msingi wa utafiti huu. Malengo yake maalum yanahusu; kufafanua rnisingi ya lugha tamathali husika kwa rnielekeo ya wanafalsafa mbalimbali, ubainishaji wa sitiari na tashbiha zinazojitokeza katika mahubiri ya dini ya kikristu katika Kiswahili, kuchanganua maana yake kiuarnilifu na kiuamalifu na mwishowe kutathrnini thamani ya rnielekeo hii ya lugha katika mawasiliano ya dini. Matumizi ya sitiari na tashbiha, na fasiri yake inahusu hasa mazingira ya muktadha na kwa hivyo nadharia za kiuamali ni mielekeo mwafaka tuliyoitumia katika uchanganuzi wa ithibati. Kupitia mbinu za unasaji na ushiriki-utazamaji, katika makanisa ya rniji mikuii mmne nchini Kenya, tulikusanya badhi ya sitiari na tashbiha zinazoturniwa katika mahubiri na kuzichanganua kiuamali, kwa kukadiria maana yake mbali mbali, kisha kuonyesha uamalifu na uarnilifu wa vitendo vitamkwa katika kufikia malengo yaliyonuiwa na mhubiri. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa wahubiri huwasilisha uwanja mkubwa wa kufasiria maana mbalimbali ya tamathali husika. Uthibiti wa .maana lengwa hutokana na ushirika wa kimaana kwenye rnisingi ya imani za washirki.en_US
dc.publisherMaseno Universityen_US
dc.titleLugha ya kitamathali katika mahubiri ya dini ya kikristuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record