• Login
    • Login
    Advanced Search
    View Item 
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    •   Maseno IR Home
    • Journal Articles
    • School of Arts and Social Sciences
    • Department of Kiswahili & Other African Languages
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi

    Thumbnail
    View/Open
    document (5).pdf (233.8Kb)
    Publication Date
    2023-05-01
    Author
    Deusdedit, Karuhanga
    Indede, Florence Ngesa
    Metadata
    Show full item record
    Abstract/Overview
    Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi. Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki. Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895). Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.
    Permalink
    https://repository.maseno.ac.ke/handle/123456789/6136
    Collections
    • Department of Kiswahili & Other African Languages [38]

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback

     

     

    Browse

    All of Maseno IRCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Statistics

    View Usage Statistics

    Maseno University. All rights reserved | Copyright © 2022 
    Contact Us | Send Feedback